Anti GBV Champion Awards
September 27

Fomu ya Ushiriki wa Tuzo za vinara katika kupambana dhidi ya ukatili wa kijinsia (GBV) Fomu 2025. WiLDAF pamoja na mtandao wa kupambana na ukatili wa kijinsia (MKUKI) wanaandaa tuzo za vinara wa kupambana dhidi ya ukatili wa kijinsia ikiwa ni sehemu ya kampeni za siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Hii ni katika kutambua na kupongeza juhudi za watu binafsi na mashirika ambayo yamechukua hatua kubwa na za kipekee katika kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii zao na Tanzania kwa ujumla.
Hivyo basi, tunaomba ushiriki wako kwenye zoezi hili kwa kujaza fomu hii https://shorturl.at/jV4Hg na kuweka mapendekezo ya vinara wanaostahili kuchukua tuzo.
Kumbuka, unaweza kupendekeza mtu au ukajipendekeza wewe binafsi.
📝 Jaza fomu: https://shorturl.at/jV4Hg
📞 Unaweza pia kupiga simu bure: 0800780070
Mwisho wa kujaza: 27/9/2025